MURSI ATANGAZA KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA
Rais Mohammad Morsi wa Misri ametangaza kuwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo itafanyika Desemba 15 mwaka huu wa 2012.
Akizungumza Jumamosi mjini Cairo wakati akipokea rasmi nakala ya rasimu ya katiba mpya, Morsi aliwahakikishia watu wa Misri kuwa atatekeleza majukumu yake kwa maslahi ya taifa.
Mapema jana, kote Misri kulifanyika maandamano ya makumi ya maelfu ya watu wanaomuunga mkono rais Morsi pamoja na rasimu mpya ya katiba inayosema nchi hiyo itaongozwa kwa msingi wa sheria za Kiislamu.
Siku ya Ijumaa wapinzani wa Morsi waliandamana mjini Cairo wakipinga katiba mpya na uamuzi wa Morsi kujiongezea madaraka.
Rais wa Misri amesema hatua yake ya kujiongezea madaraka ni ya muda mfupi tu kwa lengo la kulinda mapinduzi ya wananchi. Ameongeza kuwa katiba mpya ikipitishwa madaraka ya rais yatapungua kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO