Sunday, December 02, 2012

MAHASIMU WA AL-SHABAB WAJIUNGA NA SERIKALI YA SOMALIA


Wanamgambo wa Ahlu Sunnah Wal Jama’a wamejiunga rasmi na serikali ya Somalia na  baada ya kupigana kwa muda wa miaka miwili bega kwa bega na vikosi vya serikali dhidi ya waasi wa Al Shabab.

Akizungumza Jumamosi mjini Mogadishu, kamanda wa ngazi za juu wa wanamgambo wa Ahlu Sunnah Sheikh Mohamed Yusuf Hefow amesema kuwa wapiganaji wa kundi lake sasa wameingia katika jeshi la serikali ya Somalia.Ahlu Sunnah Wal Jama’a Somalia wanakadiriwa kuwa na wapiganaji 2000 na aghalabu ni wafuasi wa itikadi ya Kisufi. Wamekuwa wakipigana dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabab tokea mwaka 2008 baada ya wafuasi wa Al Shabab kuhujumu maeneo ya Masufi katika eneo la Galgaduud kati mwa Somalia.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO