NATO YAASISSI KITUO KIPYA CHA KIJESHI UTURUKI
Muungano wa kijeshi wa Nato umeasisi kituo kipya cha kijeshi katika mkoa wa Izmir magharibi mwa Uturuki huku muungano huo wa kujihami wa Magharibi ukiwa na mpango wa kuweka ngao ya kisasa ya makombora ya Patriot katika mpaka kati ya Uturuki na Syria. James Stavridis kamanda mkuu wa Nato amesema katika sherehe za ufunguzi wa kituo hicho cha kijeshi kuwa Nato imekuwa ikiiamini Uturuki tangu nchi hiyo iwe mwanachama. Akizungumza kuhusu kuwekwa ngao ya makombora ya Patriot huko kusini mwa Uturuki, kamanda wa Jeshi la Ardhini la Muungano wa Nato Jenerali Frederick Ben Hodges amedai kuwa hatua hiyo haina lengo la kuanzisha eneo lisiloruhusiwa kuruka ndege au mashambulizi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO