Saturday, December 01, 2012

BRAHIMI ASISITIZA UINGIALIAJI WA KIJESHI NCHINI SYRIA

Lakhdar Brahimi Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Syria ametaka uwepo uingiliaji wa kijeshi nchini humo ili kukabiliana na hali mbaya inayoendelea kushuhudiwa  nchini humo. Akizungumza mbele ya wajumbe wa  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Brahimi ameongeza kuwa, mapigano yamezidi kusambaa karibu nchi nzima ya Syria, hivyo kuna ulazima wa kuchukuliwa hatua za haraka za kuzuia maafa zaidi nchini humo. Amesema kuwa, waasi wa Syria wanasisitiza juu ya kung'atuka Rais Bashar Assad na washirika wake kabla ya kuanza mazungumzo yenye lengo la kutafuta njia za kuutatua mgogoro huo. Brahimi amesisitiza kuwa, mgogoro wa Syria ulipaswa utatuliwe kwa njia za mazungumzo, lakini hakuna matumaini ya kupatikana amani kwa njia hiyo. Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Syria amesema kuwa, kuna ulazima wa kutumwa kikosi cha kulinda amani cha umoja huo kitakachokuwa na uwezo mkubwa wa kuleta amani nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO