Saturday, December 01, 2012

RAIS WA TUNISIA ATAKA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Rais Munsif Marzouki wa Tunisia amemtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hamadi Jebali kuteuwa baraza jipya la mawaziri huku wananchi wakiendelea kuandamana wakilalamikia hali ngumu ya maisha nchini humo. Rais wa Tunisia amesema serikali ya mseto ya nchi hiyo imeshindwa kukidhi matakwa ya wananchi na kutaka kuundwa serikali mpya ndogo itakayoweza kushughulia hali ya machafuko iliyoikumba nchi hiyo sasa. Munsif Marzouki amesema chaguzi mpya zinapasa kufanyika haraka iwezekanavyo nchini humo kabla ya msimu ujao wa joto na kuitaja hali ya machafuko iliyoigubika nchi hiyo kuwa jambo lisilokubalika. Amesema serikali ya nchi hiyo ni lazima ibadilishwe ili kupatikana serikali mpya ya wataalamu na si ile inayowajumuisha wanasiasa kutoka mirengo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO