Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, amefanya ziara kuvitembelea vikosi vya jeshi la Ujerumani vilivyoko nchini Afghanistan. Gauck alikutana na vikosi vya jeshi hilo vilivyoko katika eneo la Mazar-e-Sharif, ambako kuna kituo kikubwa katika jimbo hilo.
Amewashukuru wanajeshi hao pamoja na wafanyakazi wa kutoa misaada ambao wanafanya kazi kuleta amani na demokrasia nchini humo.
Jeshi la ulinzi la Ujerumani limeanza kupunguza wanajeshi wake nchini Afghanistan, pamoja na kuongeza uwezo wake wa jumla wa kushambulia. Helikopta kadhaa chapa Tiger zimepelekwa hivi karibuni katika jimbo hilo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa majeshi ya Ujerumani kusaidiwa na helikopta zake yenyewe.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO