Watoto wawili wahanga wa mauaji ya wiki iliyopita katika jimbo la Connecticut nchini Marekani wamezikwa. Watoto wa kiume wawili wenye umri wa miaka sita, Noah Pozner na Jack Pinto , walikuwa miongoni mwa watoto 20 waliouawa wakati mtu mwenye silaha alipowafyatulia risasi katika shule ya msingi mjini Newtown Ijumaa iliyopita. Watu wazima sita ambao ni wafanyakazi wa shule hiyo pia wameuawa pamoja na mama wa mshambuliaji huyo.
Shambulio hilo la silaha limezusha mjadala kuhusu udhibiti wa silaha nchini Marekani, ambapo maseneta wawili wakiungwa mkono na kundi lenye ushawishi mkubwa linalopendelea umiliki wa silaha, wakitoa wito jana kuwapo na mabadiliko katika sheria za umiliki wa silaha.
Wakati hakutaja moja kwa moja mageuzi katika umiliki wa silaha wakati wa hotuba yake mwishoni mwa juma, rais wa Marekani Barack Obama jana alikutana na makamu wa rais Joe Biden pamoja na baraza la mawaziri kujadili njia za kuchukua.
Msemaji wa rais Obama hakutoa maelezo kamili lakini amesema mpango wake umekwenda mbali zaidi ya udhibiti wa silaha.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO