Jumuiya ya Ustawi wa Kusini mwa Afrika (SADC) imeahidi kutuma kikosi cha askari 4,000 kisichopendelea upande wowote mashariki mwa Kongo kwa lengo la kulinda amani katika eneo hilo.
Jumuiya hiyo pia imeutaka Umoja wa Mataifa uimarishe kikosi chake cha kulinda amani nchini Kongo ambacho kililazimika kuacha kuulinda mji wa Goma mwezi uliopita baada ya askari wa serikali kukimbia mji huo na waasi kusonga mbele. Hayo yameelezwa mwishoni mwa mkutano wa SADC uliofanyika mjini Dar es Salaam Tanzania ambapo pia nchi wanachama zimelaani harakati za waasi wa M23 na mashambulizi yao dhidi ya raia wa mashariki mwa Kongo.
Hata hivyo mwenyeji wa mkutano huo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema, kupelekwa askari hao huko Congo kutategemea maamuzi yatakayochukuliwa na nchi wanachama juu ya askari hao na gharama zake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO