Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti ametangaza kuwa atajiuzulu baada ya bajeti ya mwaka huu nchini humo kupasishwa, akisema kwamba hawezi tena kutawala baada ya chama cha Silvio Berlusconi kujiondoa katika serikali. Awali Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlosconi ambaye alilazimika kujiuzulu mwaka uliopita kutokana na kashfa ya ngono na madeni, alisema kwamba atagombea kuongoza tena nchi hiyo mwaka ujao. Berlusconi amesema, chama chake cha PDL kitaendelea kupinga sera za kusimamia uchumi za Monti.
Uamuzi huo wa Waziri Mkuu wa Italia wa kujiuzulu unatayarisha mazingira ya kufanyika uchaguzi wa mapema ikiwa ni mwaka mmoja tangu mwanauchumi huyo asaidie kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro mkubwa wa madeni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO