Tuesday, December 18, 2012

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA ISRAEL AJIUZULU

Waziri wa Mambo ya Nje wa Utawala wa Kizayuni wa Israel Avigdor Lieberman leo ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa wake huo na kukabidhi ofisi kwa Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu. Baada ya siku moja kutuhumiwa kwa ufisadi na uhaini, Lieberman alitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo. Wizara hiyo ya Mambo ya Nje ya Israel imetangaza kuwa, baada ya kujiuzulu Lieberman, nafasi yake itachukuliwa na Naibu wake Danny Ayalon. Kujiuzulu kwa viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni, kunakuja baada ya kushindwa na muqawama wa Palestina katika vita vya siku nane vya Ukanda wa Gaza, kushindwa ambako pia kumempelekea Waziri wa Vita wa Utawala huo kutangaza kujiuzulu. Hivi karibuni Waziri wa Utalii wa Israel, naye alitangaza kujiuzulu, kutokana na kushadidi ukosoaji dhidi yake na kukabiliwa na kashfa za uchafu wa kimaadili.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO