Idadi ya Waislamu kwenye magereza ya nchini Uingereza inazidi kuongezeka siku baada ya siku. Kwa mujibu wa taarifa ya Nick Hardwick Mkaguzi Mkuu wa jela nchini Uingereza, kila vijana watano waliofungwa kwenye jela za nchi hiyo mmoja wapo ni Muislamu. Hardwick ameongeza kuwa, katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2010 wafungwa Waislamu walikuwa ni asilimia 13 na kipindi cha mwaka 2011 hadi 2012 idadi hiyo imeongezeka na kufikia asilimia 21. Taarifa hiyo ya mkaguzi wa jela nchini Uingereza imeeleza kuwa, kila wafungwa watano Waislamu wawili kati yao walipatwa na makosa ya kupigana na utumiaji nguvu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO