Viongozi wa Libya wamesema kuwa, wamewatia mbaroni wahubiri wa Kikristo wasiopungua 50 kutoka nchini Misri ambao wameingia nchini humo kinyume cha sheria kwa lengo la kuhubiri mafundisho ya dini ya Kikristo kwa wakazi wa mji wa Benghazi nchini humo. Taarifa zinasema kuwa, wahubiri waliingia nchini humo kwa madai kuwa ni wafanyabiashara, amma makachero wa Libya waliwatia mbaroni wakati wakitoa mahubiri ya Kikristo kwenye maeneo ya mji wa Benghazi. Vyanzo vimeeleza kuwa, jamii ya Libya ni ya Kiislamu na mahubiri hayo yatasababisha ghasia na machafuko na hatimaye kupotea uthabiti wa kijamii nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO