Serikali ya Misri imelipa jeshi kuimarisha usalama na kusaidia kulinda taasisi muhimu za serikali hadi baada ya kura ya maoni ya rasimu ya katiba iliyopangwa kufanyika Disemba 15. Amri hiyo imelipa jeshi mamlaka ya kuwatia mbaroni raia wanaozusha fujo na kushirikiana na jeshi la polisi kuimarisha usalama wakati wa utekelezwaji wa kura hiyo ya maoni hadi matokeo yatakapotangaza.
Amri hiyo imetangazwa huku wapinzani wakiitisha maandamano makubwa hapo kesho Jumanne kupinga kura ya maoni ya rasimu ya katiba mpya. Hussein Abdul Ghani msemaji wa mrengo wa National Salvation Front amewaambia waandishi habari kuwa, wamekuwa wakipinga suala hilo kuanzia mwanzo wake hadi mwisho wake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO