Saturday, January 12, 2013

UHUSIANO WETU NI KWA AJILI YA WAISLAM

Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema kwamba, kuimarishwa uhusiano wa nchi yake na Iran ni kwa maslahi ya ulimwengu wa Kiislamu. Mursi amesema hayo alipokutana na Ali Akbar Salehi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran mjini Cairo, na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nchi kubwa katika eneo na yenye nafasi muhimu katika kujenga urafiki na maelewano kati ya mataifa. Vilevile Rais wa Misri amepongeza jitihada za Iran katika kutatua mgogoro wa Syria na kusema kwamba serikali ya Cairo inapinga uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Syria. Kwa upande wake Ali Akbar Salehi amesema kuwa, Iran na Misri ni nchi zinazokamilishana na kwamba Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kulipatia taifa la Misri uzoefu wake wa miaka 30. Huku akiashiria suala la Syria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, kundi la mawasiliano la pande 4 ni chaguo linalofaa kutumiwa kuutatua mgogoro wa nchi hiyo na kuongeza kwamba ana matumaini kupitia pande hizo hatua muhimu zitaweza kuchukuliwa. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO