Monday, January 14, 2013

WATU WAZIDI KUKATAA KUINGIA JESHINI ISRAEL

Suala la kupungua idadi ya watu wanaokwepa kujiunga na jeshi la utawala wa Kizayuni, ni changamoto mpya kwa viongozi wa kisiasa na kijeshi wa utawala huo haramu. Katika toleo lake la hivi karibuni, gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronot, limewanukuu viongozi wa jeshi katika utawala huo wa Kizayuni wakisema kwamba, kutokana na kupungua kila siku idadi ya watu walioko tayari kulitumikia jeshi la Israel licha ya kwamba utawala huo unahitajia idadi kubwa ya maafisa wapya wa kijeshi, kumewapelekea viongozi wa jeshi kufikiria aina mpya ya kukabiliana na tatizo hilo. Gazeti hilo la Kizayuni limekutaja kukimbia, kupungua idadi ya watoto wanaozaliwa na kuongezeka idadi ya watu wanaokimbilia nje ya Israel pamoja na kukataa kujiunga na jeshi hilo Mayahudi wenye imani za kidini, kuwa ni sababu kuu ya kupungua watu wanaojiandikisha jeshini. Katika hali hiyo sambamba na kuongezeka kwa mivutano kuhusiana na kutumikia jeshi kwa Mayahudi wenye kufuata imani za kidini huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, Kiongozi Mkuu wa Kidini wa chama cha "Shas", Kuhani Ovadia Yosef ameonya juu ya hatari ya kuongezeka idadi ya Mayahudi wenye imani za kidini wanaoikimbia Israel iwapo vijana wa Israel watalazimishwa kuingia jeshini. Katika miaka ya hivi karibuni suala la vijana kukwepa kujiunga jeshini huko Israel, limekuwa ni tatizo kubwa kiasi kwamba, vijana wengi wa Israel wanakwepa kwenda jeshini kwa kukimbilia kusomea dini, kwani kwa mujibu wa sheria za ndani huko Israel, watu wa dini hawashiriki katika harakati za kisiasa na kiuchumi, katika utawala huo na wanasamehewa kutumika jeshini. Inaonekana ni kwa sababu hiyo ndio maana hivi karibuni, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu aliwasilisha mpango wa sheria inayohusiana na utumishi jeshini, sheria ambayo ilikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Mayahudi wenye mielekeo ya kidini, hasa vyama vya kisiasa vya Yisrael Beitenu na Shas. Katika hali ya kutetea muswada wake unaowataka wanafunzi wa kidini wapatao 1300 kujiunga jeshini, Netanyahu alisema kuwa, utawala wa Kizayuni ni utawala ambao unategemea kikamilifu jeshi na kwamba, jeshi nalo linahitajia watu wajitolee kuingia jeshini. Kwa mujibu wa takwimu za vyombo vya usalama vya Israel, mwenendo wa kukwepa vijana wa Israel kujiunga jeshini, umeongezeka sana hivi sasa kiasi kwamba katika mwaka 2012 pekee  idadi ya vijana waliokwepa kujiunga jeshini ilifikia watu 2000. Aidha kwa mujibu wa takwimu za jeshi la Israel, zaidi ya asilimia 40 ya vijana waliotakiwa kujiunga jeshini walikwepa kufanya hivyo. Ahadi za urongo za viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni na kushindwa vibaya na muqawama wa Lebanon na Palestina katika vita vya mwaka 2006, 2009 na 2012 zimetajwa kuwa ni katika sababu za kushuhudiwa hali hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO