Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetishia kuichukulia Israel hatua za kisheria
katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) iwapo Tel Aviv itajenga nyumba mpya
katika maeneo ya Palestina inayoyakaliwa kwa mabavu. Riyad al Maliki Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina
amesema hayo baada ya kushiriki kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa mjini New York. Ameongeza kuwa, iwapo Israel itaendelea kujenga
vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni pamoja na mipango mingineyo katika mji
wa Baitul Muqaddas, Palestina itaifungulia mashtaka katika mahakama ya ICC kwani
haitakuwa na chaguo jingine.
Utawala wa Kizayuni wa Israel unapanga kupanua vitongozi vya walowezi wa
Kizayuni katika maeneo ya Palestina unayoyakalia kwa mabavu pambizoni mwa Quds
Mashariki, suala ambalo ni kinyume cha maazimio na sheria za
kimataifa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO