Saturday, January 12, 2013

BOMU LARIPUKA TEL-AVIV

Wazayuni wapatao 10 wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea karibu na jengo la Wizara ya Vita ya Utawala wa haramu wa Kizayuni katika mji mkuu wa Tel Aviv huko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Tukio hilo limetokea leo baada ya bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari karibu na wizara hiyo kuripuka. Duru za habari kutoka Israel zinaarifu kuwa, shambulio la mripuko huo limetekelezwa na mamafia wa Kizayuni ambao wanaipinga serikali ya utawala huo ghasibu na kwamba hadi sasa vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo. Haya yanajiri katika hali ambayo Israel inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu ambao unatazamiwa kufanyika katika wiki mbili zijazo. Kutokana na maoni ya weledi wengi wa kisiasa, uchaguzi huo unaweza kumbwaga Waziri Mkuu wa sasa wa utawala huo haramu, Benjamin Netanyahu ikiwa chama chake cha Likud kitashinndwa kupata viti vingi bungeni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO