Wednesday, January 02, 2013

CHAVEZ APATA FAHAMU ZAKE


Rais Hugo Chavez wa Venezuela ameripotiwa kupata fahamu zake baada ya kufanyiwa upasuaji wa nne kutokana na saratani nchini Cuba. Baada ya kumtembelea Rais Chavez hospitalini, naibu wake Nicolas Maduro amesema kuna maendeleo ya kiasi fulani kwenye hali ya Chavez.
Hata hivyo, Maduro alisema bado kiongozi huyo yuko kwenye hali tete sana. Chavez, mwenye umri wa miaka 58 na ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1999, alichaguliwa tena mwezi Oktoba mwaka jana kuiongoza Venezuela kwa awamu ya nne. Sherehe za kumuapisha kiongozi huyo kwa ajili ya muhula wake mpya zimepagwa kufanyika tarehe 10 Januari.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO