Shirika la kutoa huduma za Satalaiti la Eutelsat limechukua hatua zisizo za
kisheria za kukata matangazo yanayorushwa na Hispan TV ya Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran.
Siku chache zilizopita, serikali ya Uhispania katika hatua inayokinzana na
uhuru wa kujieleza ilitoa amri kwa shirika linalotoa huduma za satalaiti la
Hispasat kukata matangazo yanayorushwa na Shirika la Utangazaji la Iran kwa
lugha ya Kihispania na ile ya Kiingereza ya Press TV.
Hatua ya Hispasat ya kukata matangazo ya Televisheni za Iran imepokelewa kwa
mikono miwili na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. David A. Harris
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mayahudi wa Marekani (AJC) amesifu na kuunga
mkono uamuzi huo. David Harris ameongeza kuwa, miezi kadhaa iliyopita
kulifanyika mazungumzo na viongozi wa Uhispania juu ya kukatwa matangazo ya
kanali za televisheni za Iran katika satalaiti ya Hispasat.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO