Wapinzani wa serikali ya Mali wametishia kulipiza kisasi kwa serikali ya
Ufaransa na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na mashambulizi wanayoyafanya
nchini humo.
Taarifa iliyotolewa na wapinzani wa serikali ya Mali imeeleza kwamba,
Ufaransa na utawala wa Kizayuni wa Israel zitakiona cha mtemakuni kutokana na
hatua zao za kuwashambulia Waislamu wa maeneo ya kaskazini mwa Mali. Taarifa
hiyo imeongeza kuwa, kila mwanamgambo wa upinzani amekula kiapo cha kulipiza
kisasi cha damu za Waislamu kutoka kwa majeshi vamizi ya Ufaransa na utawala wa
Israel.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa yapata siku kumi zilizopita alitoa amri ya
kushambuliwa maeneo ya kaskazini mwa Mali, mashambulio ambayo yamelitumbukiza
eneo lote la magharibi na kaskazini mwa Afrika katika machafuko. Serikali ya
Paris imewapeleka wanajeshi wasiopungua 2,150 nchini Mali kwa lengo la
kutekeleza operesheni ya kijeshi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO