Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, utawala wa
Kizayuni wa Israel ndio unaobeba dhima ya roho za wafungwa na mateka wa
Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya utawala huo katili. Taarifa ya
Hamas sambamba na kutoa mkono wa pole kutokana na kuuawa shahidi Ashraf Abu
Dhari' mateka wa Kipalestina aliyekuwa akishikiliwa katika moja ya magereza ya
utawala huo ghasibu imesisitiza kwamba, askari magereza wa utawala huo wamekuwa
wakiwatesa mateka na wafungwa wa Kipalestina kwa adhabu na mateso mbalimbali ya
kiroho na kimwili. Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani
vitendo vya kinyama wanavyofanyiwa Wapalestina katika magereza ya Israel na
kuitaka jamii ya kimataifa pamoja na asasi za kutetea haki za bninadamu
ulimwenguni zichukue hatua za maana ili Wapalestina hao waachiliwe huru. Aidha
Hamas imetoa wito kwa asasi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa na Baraza la
Usalama la umoja huo ziushinikize utawala wa Kizayuni wa Israel ili uache
kuwafanyia unyama wafungwa na mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika
magereza ya Israel.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO