Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia zimesema
kuwa, zina azma ya kushirikiana katika uwanja wa kupambana na uhalifu wa
kimataifa yakiwemo magendo ya madawa ya kulevya na ugaidi. Hayo yameelezwa na
Ismail Ahmadi Muqaddam Mkuu wa Jeshi la Polisi la Iran na Vladimir Kolokoltsev
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Russia katika mazungumzo yao hapa mjini Tehran.
Ismail Ahmadi Muqaddam Mkuu wa Jeshi la Polisi la Iran ameashiria katika
mazungumzo hayo juu ya vitisho mbalimbali na vya pamoja na kubainisha kwamba,
Iran na Russia zina uwezo wa kitaalamu, kielimu na kivitendo katika uwanja wa
kupambana na madawa ya kulevya na ugaidi. Kwa upande wake Vladimir Kolokoltsev
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Russia amesisitiza katika mazungumzo hayo kwamba,
kuna udharura wa kupanuliwa ushirikiano wa nchi mbili hizi katika uwanja wa
usalama sambamba na kutekelezwa maafikiano ya Moscow na Tehran katika uwanja
huo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO