Afisa wa uhusiano wa kimataifa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya
Palestina Hamas ametangaza kuwa suala la kuachiwa huru mateka wa Kipalestina
wanaoshikiliwa katika jela za Israel ni moja ya vipaumbele vya Hamas na makundi
mengine ya mapambano ya Palestina.
Usama Hamdani ameeleza kuwa mateka zaidi ya elfu tano wa Kipalestina
wanashikiliwa katika jela za utawala wa Kizayuni na kwamba kuachiwa huru raia
hao ni moja ya masuala yanayozingatiwa sana na Hamas na makundi mengine ya
mapambano ya Palestina. Usama Hamdani pia amesema kuhusiana na kukusanyika kila wiki kwa Wapalestina
mbele ya ofisi ya Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani huko Ghaza kuwa, Hamas
itatekeleza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa Wapalestina walioko katika jela za
Israel wanakuwa huru na kwamba faili la mateka hao litafungwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO