Jumuiya ya Walinganiaji wa Kiislamu wa Misri imetoa wito wa kufukuzwa
mabalozi wa Ufaransa katika nchi za Kiislamu na Kiarabu. Jumuiya hiyo imetaka kufukuzwa mabalozi wa Ufaransa katika nchi hizo na
kutoa wito wa kushinikizwa Paris ili isitishe mashambulizi yake ya kijeshi huko
Mali. Jumuiya hiyo inapinga vikali uingiliaji kijeshi wa Ufaransa huko nchini
humo.
Walinganiaji wa Kiislamu wa Misri pia wameutaka Umoja wa Mataifa kutekeleza
majukumu yake mbele ya uingiliaji kijeshi wa Ufaransa huko Mali na kuishawishi
Paris isimamishe mashambulizi yake dhidi ya nchi hiyo. Rais Francois Hollande wa Ufaransa siku kumi zilizopita alitoa amri ya kuanza
vita dhidi ya makundi yanayobeba silaha huko kaskazini mwa Mali, mashambulizi
yanayotajwa kuigharimu fedha nyingi Ufaransa. Eneo la kaskazini mwa Mali
linakabiliwa na mashambulizi makubwa ya ndege za kivita za Ufaransa kwa siku
kadhaa sasa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO