Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ametumia hotuba yake ya mwaka mpya kusisitiza kuendelea kwa masuala ya uvumbuzi wa kiteknolojia nchini mwake. Bibi Merkel ameonya kuwa mwaka huu wa 2013 utakuwa mgumu zaidi kuliko ule wa 2012 ambao Ujerumani ilifanikiwa kujilinda na mzozo wa uchumi. Kauli hiyo ya Kansela Merkel inakinzana na ile iliyotolewa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaueble iliyosema kuwa nchi hiyo iko mbali sana na mtikisiko wa kiuchumi. Aidha Kansela Merkel ametoa wito wa kuwepo juhudi za kimataifa katika kuangalia masuala ya masoko, akisema kuwa bado ulimwengu haujajifunza vya kutosha kutoka mzozo wa uchumi wa mwaka 2008. Kiongozi huyo aliwashukuru pia wanajeshi, askari polisi na wafanyakazi wa umma kwa juhudi zao za kuiweka nchi na baadhi ya maeneo duniani katika hali ya usalama.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO