Monday, January 21, 2013

IRAN YATENGENEZA HELIKOPTA YA KUBEBA WATU 8


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ufundi cha Khoja Nasruddin Tusi cha nchini Iran amesema kuwa, wataalamu wa Chuo Kikuu hicho wametengeneza helikopta ya taifa yenye uwezo wa kubeba watu wanane. Bw. Majid Qasemi ametangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, kazi ya kubuni na kutengeneza helikopta hiyo ya taifa imechukua muda wa miaka miwili.
Amesema hayo katika sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa Wahandisi wa Masuala ya Ufundi na kuongeza kuwa, Chuo Kikuu hicho kimekuwa kikitekeleza miradi mbalimbali ya kitaifa ikiwa ni pamoja na kutengeneza ndege aina ya Shabah inayotumia teknolojia na utaalamu maalumu wa kukwepa kuonekana na rada, kutengeneza satalaiti na miundo mbalimbali ya magari ya kisasa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO