Russia
imeanza kufanya mazoezi makubwa zaidi ya jeshi lake la majini katika bahari za
Mediterranean na Bahari Nyeusi karibu na maji ya Syria ambayo inakabiliwa na
mashambulizi ya magenge ya waasi. Hayo ni mazoezi makubwa zaidi ya Jeshi la
Majini kuwahi kufanywa na Russia kwa makumi ya miaka. Taarifa rasmi ya Wizara
ya Ulinzi ya Russia imesema kuwa, luteka hiyo ya kijeshi inafanyika katika
utaratibu wa Vikosi vya Ulinzi vya Russia wa mwaka 2013 wa kujiimarisha
kiulinzi na kuzingatia zaidi suala la kufanya kazi kwa pamoja vikosi vya nchi
hiyo kutoka makundi mbalimbali ya manowari zake zinapokuwa kwenye maji ya
mbali.
Maneva hayo ya Jeshi la Majini la Russia yataendelea hadi tarehe
29 mwezi huu wa Januari kwa kufanya mazoezi mbalimbali na kujaribisha silaha na
mbinu tofauti za kivita. Russia inazilaumu nchi za Magharibi kwa kuchochea
mauaji na uasi nchini Syria ambayo imekuwa ikishuhudia machafuko tangu katikati
ya mwezi Machi 2011. Raia wengi na maafisa usalama wa serikali ya Syria
wameuawa katika machafuko hayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO