Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, amesema kuwa, Russia imekubali kusaidia usafiri wa wanajeshi katika maeneo mbalimbali ya Mali kwa ajili ya kupambana na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo.
Laurent Fabius amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa leo na redio ya Europe 1 na kuongeza kuwa, sehemu moja ya usafiri wa wanajeshi katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika utafanywa na Waafrika wenyewe, sehemu nyingine itafanywa na nchi za Ulaya na sehemu nyingine itafanywa na Canada. Amesema, Russia nayo imependekeza kutoa usafiri kwa wanajeshi hao.Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hiyo ni ishara ya awali inayoonesha uwezekano wa Russia kuiunga mkono Ufaransa katika operesheni yake dhidi ya waasi wa Mali ambao wameyateka maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo tangu mwezi Aprili 2012.
Jana Rais Francois Hollande wa Ufaransa alisema kuwa Paris itaendelea na uingiliaji wake wa kijeshi katika mgogoro wa Mali hadi utakapotokomeza kikamilifu kile alichokitaja kuwa ni vitendo vya ugaidi katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO