Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kuwa utawala huo hauna uwezo wa kusimamisha mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani. Akizungumza Jumatano mjini Tel Aviv katika mkutano na ujumbe wa lobi ya Kizayuni Marekani, Netanyahu amekiri kuwa hata Israel ikitumia mbinu za kijeshi haiwezi kusimamisha mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani. Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa hivi karibuni wa bunge katika utawala huo, Netanyahu alitumia kadhia ia ya nyuklia ya Iran kujaribu kupata viti vingi lakini hakufaulu bali alipata pigo kubwa kuliko uchaguzi uliopita.
Netanyahu ameutaja mwaka wa 2013 kuwa nyeti kuhusu kadhia ya nyuklia ya Iran na ameitaka lobi ya Kizayuni Marekani kutumia ushawishi wake kuishinikiza Marekani izuie mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO