Wednesday, January 16, 2013

JAPAN NA MAREKANI ZAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA


Ndege za kijeshi za Japan na Marekani zimefanya mazoezi ya pamoja, siku chache baada ya ndege za Japan na China kukaribiana karibu na visiwa vinavyozozaniwa katika bahari ya China Mashariki. Mazoezi hayo  ya siku tano yanafanyika juu ya bahari karibu na kisiwa cha Shikoku, cha nne kwa ukubwa nchini Japan.
Yanakuja pia wiki chache baada ya waziri mkuu mbabe, Shinzo Abe, kuchukua madaraka, na kuahidi kuimarisha ushirikiano na Marekani katika masuala ya ulinzi, na kuchukua msimamo mkali dhidi ya China. Mvutano umeongezeka kati ya China na Japan kuhusu umiliki wa visiwa vijulikanavyo kama Senkaku nchini Japan na Diaoyu nchini China. Kuna taarifa kwamba kwamba Japan ilifanya mipango ya dharura kuzipeleka ndege zake za kivita katika eneo la visiwa hivyo Alhamisi iliyopita, kuzuia ndege za China ambazo zilikuwa kwenye anga iliyo karibu ya visiwa hivyo inayodhibitiwa na Japan.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO