Monday, January 14, 2013

MUUNGANO WA TANZANIA NI KWA MADHARA YA ZANZIBAR


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa, mfumo wa hivi sasa wa serikali mbili nchini Tanzania umekuwa na madhara makubwa ya kiuchumi na kisiasa kwa Wazanzibari na kusisitiza kuwa, koti la Muungano huo linawabana sana Wazanzibari na wanahitaji kubadilishiwa koti jengine la kiasi chao. Maalim Seif amesema hayo leo nyumbani kwake Mbweni, kisiwani Unguja mbele ya tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya ya Tanzania inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar pia amesema kutokana na hali halisi ya mambo ilivyo hivi sasa, Muungano wa Mkataba ndio anaohisi unafaa kati ya pande mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani Tanganyika na Zanzibar. Maalim Seif ni kiongozi wa kwanza mashuhuri kukutana na tume hiyo na ameongeza katika maoni yake kwa kusema kuwa mfumo wa hivi sasa wa serikali mbili nchini Tanzania haufai kwani umetawala kwa miaka 49 na umeshindwa kutatua kero za muungano huo bali hata umekuwa ukiongeza idadi ya kero hizo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO