Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti la The Times la utawala haramu wa
Israel unaonyesha kuwa idadi kubwa ya Wazayuni hawatilii maanani porojo za kila
siku za Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwamba Iran inakaribia kumiliki silaha za
nyuklia.
Uchunguzi huo umeonyesha kwamba, asilimia 43 ya Wazayuni wanatiwa wasiwasi na
hali mbaya ya kiuchumi na ukosefu wa ajiri kwa vijana wa Israel. Netanyahu
amejaribu kufunika ukweli huo kwa kuwahadaa Wazayuni kwamba tishio kubwa
linalowakabili ni Iran na kwamba miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya
Tehran ina malengo ya kijeshi.
Duru za habari zinaripoti kwamba, washauri wa Benjamin Netanyahu wamemtaka
abadili stratejia yake na kuangazia changamoto zinazoukabili utawala huo ghasibu
badala ya kupiga domo kuhusu Iran iwapo anataka kupata ushindi kwenye uchaguzi
wa wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO