Kundi la Misaada la Madaktari wasio na Mipaka wa Ufaransa
limeeleza kuwa timu yake ya huduma za kitiba imezuiwa kufika katika maeneo
yaliyoathiriwa na mgogoro unaondelea sasa huko Mali. Taasisi hiyo isiyo ya
kiserikali ya Ufaransa imesema kuwa imekuwa ikiwasiliana na maafisa wa Mali na
raia wa nchi hiyo tangu Januari 14 na pia na serikali na jeshi la
Ufaransa ili kuruhusiwa kutuma timu yake ya madaktari katika mji wa Konna
huko katikati mwa Mali.
Kundi la Madaktari wasio na
Mipaka la Ufaransa limesema kuwa timu yake ya madaktari imeshindwa kuhudumia
majeruhi katika medani za vita licha ya kundi hilo kutoegemea upande wowote,
tangu vikosi vya Mali na Ufaransa vianzishe oparesheni ya kijeshi huko Mali
hivi karibuni. Januari 11 mwezi huu Ufaransa ilianzisha uingiliaji kijeshi huko
kaskazini mwa Mali kwa kisingizio cha kutaka kuwazuia waasi kusonga mbele
nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO