Saturday, January 12, 2013

MAPIGANO MAPYA YAZUKA IRALAND

Mapigano yameripuka upya katika mji mkuu wa Ireland ya kaskazini-Belfast kati ya vikosi vya polisi na waandamanaji wanaoiunga mkono Uingereza.Waandamanaji walivurumisha mawe na chupa na kulitia moto basi moja.Vikosi vya usalama vilitumia mabomba ya maji na risasi za mpira kuwatimua waandamanaji.Kwa mujibu wa Polisi, askari kadhaa wamejeruhiwa.Mapigano yameripotiwa pia katika miji jirani ya Carrickfergus na Newtownabbey.Chanzo cha mapigano haya ni maandamano yanayoendelea tangu wiki kadhaa sasa dhidi ya uamuzi wa serikali ya mji unaotaka bendera ya Uingereza inayopepea tangu karne kadhaa katika jengo la serikali hiyo,iwe ikipandishwa  kwa matukio maalum tu.Wafuasi wa Kiprotestanti wanaopendelea Ireland ya Kaskazini iendelee kuwa sehemu ya Uingereza wanauangalia uamuzi huo kuwa ni sawa na kuridhia madai ya Wakatoliki wanaotaka Ireland ya Kaskazini ijitenge na Uingereza.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO