Saturday, January 12, 2013

JESHI LA UFARANSA LAJARIBU KUOKOA MATEKA WAO SOMALIA

Opereshini ya kijeshi ya Ufaransa kutaka kumuokoa mateka wa Kifaransa nchini Somalia imeshindwa.Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa ameuwawa katika opereshini hiyo-hayo ni kwa mujibu wa duru za waasi wa Kisomali wanaofuata itikadi kali,zilizolifikia shirika la habari la Ufaransa AFP mjini Nairobi."Wafaransa hawakukipata walichokitaka,kwa sababu mateka hajakuwepo katika eneo hilo" walilolishambulia usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi"   msemaji wa Al Shabab Abdulaziz Abu Musab ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ufaransa,ikihojiwa na shirika la AFP kutoka Paris,haikutaka kusema chochote kuhusu ripoti hiyo.Mtumishi wa idara ya upelelezi ya Ufaransa anashikiliwa na waasi wa Al Shabab nchini Somalia tangu Julai 14 2009. Alitekwa nyara mjini Mogadishu pamoja na mwenzake aliyeachiwa huru mwezi mmoja baadae.Na habari za hivi punde zinasema waasi wa Al Shabab wamemuuwa mateka huyo wa kifaransa

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO