Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufilipino imetangaza kuwa watu wenye silaha
wamewauwa wafanyakazi sita raia wa nchi hiyo huko katika kiwanda cha gesi asilia
nchini Algeria. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufilipino Raul Fernandez amesema kuwa
vifo vya wafanyakazi hao sita raia wa Ufilipino vilitokea baada ya kutekwa nyara
kwenye kiwanda hicho cha gesi na zaidi vilisababishwa na majeraha ya risasi na
athari za milipuko.
Wakati huo huo Algera imetahadharisha kuwa idadi ya vifo vya mateka katika
kiwanda cha gesi nchini humo vitaongezeka. Hadi sasa mateka wasiopungua 48
wanakadiriwa kuwa wameuawa katika kituo cha gesi cha Sahara huku wengine
wanaokaribia 20 wakiwa hawajulikani walipo. Vikosi vya jeshi la Algeria jana vilisema kuwa vimegundua viwiliwili vya
mateka 25 na kuwatia nguvuni watekaji nyara watano katika kiwanda cha gesi cha
In Amenas kilichopo katika jangwa la Sahara siku moja baada ya kulivamia eneo la
kiwanda hicho linaloendelea kushikiliwa na waasi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO