Rais Michel Suleiman wa Lebanon amesema kuwa, nchi yake itaendelea na juhudi
zake kwa shabaha ya kuhakikisha linaundwa taifa huru la Palestina, mji mkuu wake
ukiwa Baytul Muqaddas. Akizungumzia mashinikizo yanayofanywa na utawala haramu
wa Kizayuni kwa ajili ya kuzuia kuundwa kwa taifa hilo Michel Suleiman amesema,
kuundwa kwa taifa la Palestina kutapelekea kuimarika demokrasia, uadilifu na
kumaliza kabisa uvamizi wa Waisrael katika eneo. Aidha Rais huyo wa Lebanon
amesisitiza juu ya haki ya kurejea wakimbizi wote wa Kipalestina katika ardhi
zao zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Akizungumzia mgogoro wa nchi jirani ya
Syria, Rais Michel Suleiman wa Lebanon amesema kuwa, lazima zifanyike juhudi za
ziada zitakazosaidia kuanza kwa mazungumzo ya kisiasa na kumaliza hali
mchafukoge inayoendelea katika nchi hiyo ya Kiarabu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO