Saturday, January 12, 2013

PERES AKIRI ARAFAT ALIULIWA


Rais wa utawala ghasibu wa Israel Shimon Peres amekiri kwa mara ya kwanza kwamba kiongozi wa zamani wa Serikali ya Ndani ya Palestina Yasser Arafat aliuawa na hakufa kutokana na maradhi ya kawaida. Tovuti ya Palestine Alyoum imeripoti kuwa, Shimon Peres amesema Arafat hakupaswa kuuawa na kwamba kulikuwepo uwezekano wa kufanya kazi naye. Rais wa Israel amesema, kuuawa kwa Yasser Arafat kumeifanya hali ya mambo iwe ngumu zaidi.
Matamshi hayo ya Shimon Peres ni sawa na kukiri waziwazi kwamba  utawala ghasibu wa Israel ulihusika katika kumuua kiongozi wa zamani wa Palestina Yasser Arafat. Yasser Arafat alifariki dunia mwaka 2004 katika hospitali moja ya kijeshi nchini Ufaransa kutokana na sumu. Kifo cha Arafat kilitokea baada ya kuzingirwa na Israel kwa kipindi cha miaka miwili katika makazi yake huko Ramallah.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO