Saturday, January 12, 2013

YEMEN WAANDAMANA MJINI SANAA


Wananchi wa Yemen wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu Sanaa wakitaka kuanza mazungumo ya maridhiano ya kitaifa na kushtakiwa maafisa wa utawala wa zamani wa nchi hiyo. Waandamanaji wamelalamikia serikali kushindwa kukidhi matakwa yao baada ya kupinduliwa dikteta Ali Abdallah Saleh nchini humo. Pia wamemtaka Rais Abdurabuh Mansur Hadi kushughulikia matatizo ya jeshini na ukosefu wa usalama kabla ya kufanya mazungumo ya maridhiano ya kitaifa.
Licha ya rais wa Yemen kuwaahidi wananchi kulifanyia marekebisho jeshi na taasisi za serikali lakini bado kuna wafuasi wa utawala wa zamani wa nchi hiyo wanaoshika nyadhifa muhimu kwenye taasisi hiyo.    

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO