Monday, January 21, 2013

QATAR YAISAIDIA ISRAEL KWA MAMILIONI YA DOLA

Tzipi Livni Kiongozi wa chama cha 'Harakati ya Israel'  amesema kuwa, serikali ya Qatar imetoa kiasi cha dola milioni tatu kumsaidia Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho Jumanne tarehe 22 Januari. Livni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Israel ameongeza kuwa, chama cha Yisrael Beytenu kinachoongozwa na Avigdor Lieberman Waziri wa zamani wa Mambo ya Nchi za Nje wa Israel nacho pia kimepokea dola milioni mbili na nusu kutoka serikali ya Qatar ikiwa ni msaada wa kampeni ya uchaguzi mkuu huo. Kwa upande mwengine, Kanali ya Kwanza ya Televisheni ya Israel imetangaza juu ya kuwepo mahusiano ya karibu kati ya Livni na mke wa Emir wa Qatar. Kwa miaka kadhaa sasa Qatar imekuwa na mahusiano ya kibiashara na mashirika ya Kizayuni, na mashirika hayo yamekuwa na ofisi zake nchini humo. Mashirika hayo yamekuwa yakitumiwa kama wenzo wa kuwepo mahusiano ya kisiasa kati ya pande mbili na kuandaa safari za pande mbili za viongozi wa Qatar na utawala wa Kizayuni wa Israel. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO