Watu
wanane wameuawa katika hujuma ya hivi karibuni ya ndege isiyo na rubani
(drone) ya Marekani huko Yemen katika mkoa wa Marib. Walioshuhudia wanasema
hujuma hiyo imejiri Jumamosi usiku katika bonde la Abeida . Maafisa wa Jeshi la
Yemen wamethibitisha kutokea hujuma hiyo lakini hawakutoa maelezo zaidi. Mara
kwa mara ndege zisizo na rubani za Marekani hutekeleza mashambulizi katika
maeneo kadhaa ya Yemen kwa kisingizio cha kupambana na magaidi. Hata hivyo
wahanga wakuu wa hujuma hizo za Marekani ni raia wakiwemo wanawake na watoto wasio
na hatia. Marekani inatekeleza hujuma za ndege zisizio na rubani katika nchi
kadhaa za Kiislamu kama vile Afghanistan, Pakistan na Somalia kwa kisingizio
hicho hicho cha kupambana na ugaidi lakini wahanga wakuu huwa ni raia. Marekani
imetangaza kuwa tayari kutumia ndege zake hizo za kivita huko Mali ambayo pia
ni nchi ya Kiislamu. Wataalamu wanasema hujuma hizo za ‘Drone’ ni ukiukaji wa wazi wa
sheria za kimataifa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO