Laurent Fabius Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa ameeleza matumaini
ya kwamba mazungumzo ya amani kati ya Wapalestina na Wazayuni yataanza haraka
iwezekanavyo. Akiashiria uchaguzi wa bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Fabius
amesisitiza kuwa, uongozi ujao wa utawala huo unapasa kuanzisha mazungumzo
haraka iwezekanavyo ya kutatua mgogoro na Wapalestina. Ameongeza kuwa, mwaka wa
2013 unapasa kuwa mwaka wa kupatikana amani katika eneo la Mashariki ya
Kati.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa amesema moja kati ya masuala
muhimu ya eneo la Mashariki ya Kati ni mapigano ya mara kwa mara kati ya
Wazayuni na Wapalestina, jambo ambalo halikuzumgumzwa hata kidogo kwenye kampeni
za uchaguzi wa Israel. Magazeti ya utawala wa Israel wiki zilizopita yalielezea mpango
utakaosimamiwa na Ufaransa na Uingereza wenye shabaha ya kuanzishwa tena
mazungumzo ya amani ambayo yalikwama miaka miwili iliyopita, baada ya utawala wa
Israel kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za
Wapalestina
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO