Tunisia imeimarisha hali ya usalama katika mipaka kati ya nchi hiyo na Libya kufuatia mshambulizi ya watu wenye silaha dhidi ya mipaka ya nchi hiyo.Vikosi vya usalama vya Tunisia vimejiweka tayari kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi hiyo baada ya Walibya wawili wenye silaha kukishambulia kituo cha walinzi wa mpakani cha Tunisia huko kusini mashariki mwa nchi hiyo. Walibya wawili waliokuwa na silaha huku wakiwa wamevalia sara za jeshi jana waliwasili Tunisia na kuelekea katika kituo cha ulinzi cha mpaka wa Tunisia ambako walikabiliwa na mashambulizi ya risasi ya walinzi wa mpakani wa Tunisia na hatimaye kutiwa mbaroni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO