Gazeti
la New York Times linalochapishwa nchini Marekani limeandika kuwa Ufaransa
imeanzisha mchezo hatari nchini Mali. Gazeti hilo limeongeza kuwa vita vya Mali
ni kitu ambacho hakikutarajiwa na Rais wa Ufaransa Francois Hollande, kwa
sababu Paris ilitarajia kuwa mashambulio yake ya hivi karibuni huko Mali
yangevifanya vikosi vya wapinzani virudi nyuma lakini badala yake uingiliaji
huo umerefusha na kuzifanya tata zaidi operesheni za kijeshi na harakati za
kidiplomasia kiasi cha kuwafanya wakosoaji wa Hollande waufananishe mgogoro wa
Mali na vita vya Vietnam au Afghanistan. Wakati huohuo Rais wa zamani wa
Ufaransa Giscard d'Estaing naye pia amemtahadharisha Rais wa nchi hiyo Francois
Hollande na hatari ya operesheni ya kijeshi nchini Mali. Giscard d'Estaing
amesema yeye anaitakidi kwamba operesheni ya aina hiyo itaibua hisia za chuki
na uadui miongoni mwa raia wa Mali. Aidha ametahadharisha juu ya kile
alichoeleza kuwa ni kudhihiri kwa ukoloni mpya.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO