Wanamgambo nchini Algeria wanasema wamefanikiwa kuzima shambulizi la Jeshi la
Algeria lililokuwa na lengo la kuwanusuru makumi ya raia wa kigeni waliotekwa
nyara jana wakiwemo raia wa Ufaransa, Uingereza na Marekani. Imearifiwa kuwa, Jumatano usiku wanajeshi wa Algeria walijaribu kuingia
katika kiwanda cha kusafisha gesi asilia katika mji wa In Amenas mashariki mwa
nchi hiyo ambako wanamgamabo hao wanawashikilia makumi ya raia wa kigeni.
Mapema jana Jumatano alfajiri wanamgambo 20 waliokuwa na silaha nzito nzito
walishambulia basi ambalo lilikuwa limewabeba raia wa kigeni wafanyao kazi
katika kiwanda cha gesi. Katika tukio hilo raia mmoja wa Uingereza na mwingine
wa Ufaransa waliuawa na wengine 41 kutekwa nyara. Raia wengine wa kigeni
waliotekwa nyara katika tukio hilo ni kutoka Ireland, Japan na Norway.
Wanamgambo hao wanasema kwamba watawaachilia huru mateka hao salama salimini kwa
sharti la Ufaransa kusitisha mashambulizi yake ya kijeshi nchini Mali.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO