Mshauri wa Rais Barack Obama wa Marekani kuhusu masuala ya ugaidi, John
Brennan amesema mbinu zinazotumiwa na CIA kuwasaili washukiwa wa ugaidi ni
kinyume cha sheria za kimataifa na mkataba wa Geneva. Brennan ameiambia kamati
ya bunge kuhusu usalama kwamba katika kipindi cha utawala wa George Bush,
washukiwa wa ugaidi waliteswa na haki zao kukiukwa wakati wa kusailiwa na
maafisa wa CIA.
John Brennan ambaye amependekezwa kuchukua uongozi wa CIA amesema akipata
nafasi hiyo atafanya juhudi kuona haki za binadamu na sheria za kimataifa
zinaheshimiwa wakati wa kuwasaili washukiwa wa ugaidi.
Wakati wa utawala wa Busha, picha za aibu za jinsi maafisa wa Marekani
walivyokuwa wakiwatesa washukiwa wa ugaidi ziliamsha hasira za walimwengu na
kuzusha maandamano makubwa katika nchi mbalimbali duniani kulaani unyama
huo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO