Thursday, January 17, 2013

IRAN YATUMA MELI ZA KIVITA BAHARI YA MEDITERRANEAN

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran Admeli Habibollah Sayyari amesema msafara wa 24 wa manowari za kivita za Jamhuri ya Kiislamu utaelekea katika Bahari ya Mediterranean hivi karibuni.
 Akizungumza Jumatano, Admeli Sayyari amesema msafara huo wa meli za kivita utalinda doria eneo la kaskazini mwa Bahari ya Hindi, Ghuba ya Aden, Bab-el-Mandeb, Bahari ya Sham, Mfereji wa Suez na Bahari ya Mediterranean kwa muda wa miezi mitatu.
Kamanda huyo ameongeza kuwa msafara wa 23 wa manowari za kivita za Jamhuri ya Kiislamu utarejea nchini wiki ijayo. Akiashiria mazoezi ya hivi karibuni ya jeshi la wanamaji, Admeli Sayyari amesema maneva hiyo ilionyesha uwezo mkubwa wa jeshi la wanamaji la Iran katika kukabilina na tishio lolote dhidi ya maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO