Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas nchini Iran amesisitiza kuwa, hatakati hiyo kamwe haitautambua rasmi utawala wa Kizayuni wa Israel. Ali Barakah ameongeza kuwa, suala la kuafiki kuundwa nchi mbili katika ardhi za Palestina, linamaanisha juu ya kuutambua rasmi utawala wa Israel. Amesisitiza kuwa, kamwe Hamas haitautambua utawala wa Kizayuni wa Israel. Ameongeza kuwa, kuundwa nchi huru ya Palestina katika mipaka ya mwaka 1967 ni jambo lisilokubaliwa na Hamas na kwamba harakati hiyo haitafumbia macho hata shubiri moja ya ardhi ya Palestina. Barakah amesema kuwa, utawala wa Kizayuni ni utawala ghasibu ambao haufungamani hata kidogo na sheria za kimataifa. Mwakilishi wa Hamas nchini Iran amewataka Wapalestina kuhifadhi umoja na mshikamano wao sanjari na kuitaka jamii ya kimataifa kuwasaidia wananchi wa Palestina katika kujipatia haki zao kutoka kwa maghasibu wa Kizayuni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO