Sunday, February 10, 2013

LIEBERMAN; HAKUNA AMANI NA WAPALESTINA

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel, Avigdor Lieberman amesema hakuna uwezekano wowote wa kuwepo makubaliano ya kudumu ya amani kati ya utawala huo ghasibu na Palestina. Liebaman amesisitiza kuwa mgogoro wa Wazayuni na Wapalestina hauwezi kutatuliwa lakini unaweza kudhibitiwa. Matamshi hayo yameikasirisha Mamlaka ya Ndani ya Palestina ambapo msemaji wa Mahmoud Abbas amesema kwamba Tel Aviv imeonyesha wazi haina nia ya kuona amani inapatikana Mashariki ya Kati. Lieberman mwenye misimamo ya kufurutu ada amesema matakwa ya Wapalestina ya kupewa uhuru wa kujitawala ni ya kiwendawazimu na kwamba hilo halitafanyika. Hii ni katika hali ambayo, ikulu ya White House ya Marekani imetangaza kwamba Rais Barack Obama atazuru Israel kwa mara ya kwanza tangu aanze kuhudumia kipindi cha pili cha uongozi wake. Obama pia atatembelea ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO