Maelfu ya watu wamekusanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran pamoja na miji mingine katika maadhimisho ya miaka 34 tangu kufanyika kwa mapinduzi ya kiislamu yaliyoutoa madarakani utawala wa Shah uliokuwa unaungwa mkono na Marekani. Mjini Tehran makundi ya watu wameonekana wakipeperusha bendera za Iran pamoja na picha za kiongozi wa mapinduzi hayo Ayatollah Ruhollah Khomeini wakielekea katika viwanja vya Azad vinavyujulikana kama viwanja vya uhuru. Waandamanaji pia wamesikika wakitoa ujumbe unaosema "kifo kwa Israel" na "kifo kwa Marekani" katika safari yao kuelekea viwanja hivyo ambapo Rais Mahmoud Ahmadinejad anatarajiwa kuhutubia. Maadhimisho haya yanaikumbuka siku ya tarehe 11 mwezi Februari miaka 34 iliyopita, pale jeshi lilipoungana na wananchi na kumuondoa madarakani utawala wa zamani wa mfalme Mohammad Reza Pahlavi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO